Dodoma FM
TANZIA: PCMA wamlilia Askofu Mondeya
18 October 2024, 8:04 pm
Na Nazael Mkude.
Wachungaji na waamini wa kanisa la PCMA Mkoani Dodoma wamepokea kwa masikitiko kifo cha Askofu Mkuu Dr. Mondea Kabeho
Katibu Mkuu wa Kanisa la hilo Patrick Kajila anaelezea jinsi msiba huo ulivyotokea wakati wa ibada ya kuwafariji wafiwa iliyofanyika katika kanisa hilo Mtaa wa Nzuguni A.
Aidha waombolezaji wamemuelezea marehemu kuwa alikuwa ni mtu wa watu na mpenda haki na atakumbukwa daima kwa mazuri yake.
Mazishi ya mwili wa aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la PCMA Tanzania yatafanyika siku ya Oct. 18 2024 jijini Dar es Salaam majira ya mchana.