Dodoma FM

Darasa tembezi hamasa kujiandikisha daftari la mpigakura Dodoma

16 October 2024, 7:28 pm

Na Mindi Joseph

Ubunifu wa matumizi darasa tembenzi katika Mkoa wa Dodoma umehamasiha kwa kiwango kikubwa wananchi kujitokeza kujiandikisha daftari la mppiga kura.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyerere Kata ya Mpunguzi Bwn. Eliaton Shadrack anaelezea juu ya mwitikio wa wananchi baada ya darasa temebezi kufika katika kata hiyo.

Pichani Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyerere Kata ya Mpunguzi Bwn. Eliaton Shadrack akiwa ndani ya darasa temebezi
Sauti ya Bwn. Eliaton Shadrack

Baadhi ya wananchi waliofikiwa na darasaa  hilo wamesema  kuwa darasa hilo  limechangia kwa kiwango kikubwa wananchi kuwa na mwitikio kujiandikisha kama wanavyoeleza wananchi wa kata ya Mpunguzi.

Pichani wanachi akielezea jinsi alvyohamasika kujiandikisha daftari la mpigakura
Sauti za wananchi
Pichani wanachi akihamasiha kujiandikisha daftari la mpigakura

Gari la Darasa Tembezi linapakia abiria bure kwa lengo la kuelimisha kuhusu uandikishaji wa daftari la makazi kuelelea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na  kuwapatia vyeti abiriawanaotoa ushirikiano wa kuuliza na kujibu maswali pamoja na kutoa maoni kwa namna ambavyo wameelewa zoezi linaloendelea.