Dodoma FM

Kibakwe jitokezeni kujiandikisha!

16 October 2024, 7:28 pm

Na Steven Noel.

Mbunge wa Jimbo la kibakwe  na waziri  Ofisi ya Rais menejiment  ya utumishi wa umna na utawala bora Mhe. George Simbachawene  amewahimiza wananchi wa Kibakwe kujitokeza kujiandikisha katika daftari la mpiga kura.

Mara baada ya kujiandikisha, Waziri Simbachawene alitumia fursa hiyo kuwasihi vijana kuweza kujiandikisha  ili wawe na sifa za kupiga kura  siku ya Novemba 27 na kutawataka wasimamizi kuendelea kutoa elimu ya uchaguzi.

Mbunge wa Jimbo la kibakwe  na waziri  Ofisi ya Rais menejiment  ya utumishi wa umna na utawala bora Mhe. George Simbachawene akionga na wanachi mara baada ya kujiandikisha.
Sauti ya Mhe. George Simbachawene

Msimamizi wa uchaguzi Katika Wilaya ya Mpwapwa Bi.  Mwanahamiis Ally  ambae ni Mkurugenzi Mtendaji  Halmashauri ya Mpwapwa aliendelea kuwahamasisha  wakazi wa Kibakwe kujitokeza kujiandikisha.

Aidha  mwenyekiti wa halmashauri hiyo George Fuime alisisitiza umuhimu wa vijana kujitokeza kujiandikisha  kwa mustakabali  wa maisha yao ya sasa na badae

 Mwenyekiti wa halmashauri ya Mpwapwa George Fuime akihamasisha vijana kujiandikisha
Sauti ya Bwn. George Fuime