Dodoma FM

Bonanza Kuhamasisha uandikishaji lafana Mpwapwa

11 October 2024, 7:25 pm

Na Steven Noel.

Wananchi Wilayani Mpwapwa  wamehamasika kwa kiwango kikubwa kuitikia wito  kujiandiksha daftari la mpiga kura.

Akishiriki bonanza maalumu la uhamasishaji zoezi la uandikishaji daftari la mpiga kura, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt Sophia Mfaume Kizigo ameambatana na viongozi wa Halmashauri hiyo kuungana na wananchi waliojitokeza kwa wingi katika bonanza hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt Sophia Mfaume Kizigo akihutubia wananchi katika bonanza la uhamasishaji daftari la mpiga kura.
Sauti ya Dkt Sophia Mfaume Kizigo

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bi. Mwanahamisi Ali anaelezea idadi ya wananchi wanaotarajiwa kuandikishwa pamoja na idadi ya vituo vitavyotumika katika zoezi  hilo.

Pichani Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bi. Mwanahamisi Ali
Sauti ya Bi. Mwanahamisi Ali

Diwani wa Wilaya ya Mpwapwa mjini pamoja na wananchi wanaeleza juu ya uelewa wao ulivyokuwa kabla ya kuanza zzoezi la kujiandikisha katika daftari la mpiga kura.

Pichani Diwani wa Wilaya ya Mpwapwa mjini
Sauti za wananchi
Pichani mwananchi akieleza akuelewa dhana ya kujiandikisha daftari la mpiga kura

Bonanza hilo lilihudhriwa na wadau mbalimbali ikiwemo waendesha boda boda, wanafunzi , viongozi wa halmashauri pamoja na wanachi . Bonanza hilo limebeba ujumbe wa kaulimbiu MKUMBUSHE JIRANI YAKO.

Pichani Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt Sophia Mfaume Kizigo akiwa na washiriki wa bonanza la uhamasishaji daftari la mpiga kura.