Dodoma FM

Misaada ni muhimu vituo vya yatima kujiendesha

9 October 2024, 6:24 pm

Na Niza Mafita.

Kituo cha kulelea watoto yatima cha Bicha ni moja ya vituo kinavyokabiliwa na changamoto ya mahitaji ya chakula pamoja na malazi.

Mwalimu wa kituo hicho Bwn. Mikidadi Ally amebainisha hayo wakati akipokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka kwa Katibu wa Bakwata na Baraza la Masheikh Mkoani Arusha Sheikh Abdalah Saidi Chudi.

Mwalimu wa kituo cha Bicha Bwn. Mikidadi Ally
Sauti ya Bwn. Mikidadi Ally

Aidha Sheikh Abdalah Saidi Chudi anaeleza sababu za kutoa msaada huo katika kituo hicho na kuhimiza wadau kujitokeza kusaidia ujenzi wa bweni katika kituo hicho lililoungua moto mwaka 2023.

Katibu wa Bakwata na Baraza la Masheikh Mkoani Arusha Sheikh Abdalah Saidi Chudi
Sauti Sheikh Abdalah Saidi Chudi
Pichani ni mabaki ya bweni la kituo cha kulelea watoto yatima cha Bicha baada ya kuungua moto 2023