Dodoma FM

‘Skanka’ hatari kwa magojwa ya afya ya akili kwa wasichana Dodoma

8 October 2024, 6:39 pm

Na Mariam Matundu.

Wasichana jijini Dodoma wapo hatarini kupata magojwa ya afya ya akili kutokana na matumizi makubwa ya dawa za kulevya aina ya ‘skanka’.

Akiwa katika mahojiano na Mariam Matundu mtangazaji wa Dodoma TV, Mkurugenzi wa taasisi ya Recovery Youth With Vision Bwn. Elianza Ngoda ametaja sababu ya matumizi hayo makubwa ya dawa za kulevya kwa wasichana ni pamoja na jiografia ya Mkoa wa Dodoma kuwa  inachagiza ongezeko hilo.

Pichani Bwn. Elianza Ngoda akieleza jinsi wasichana Dodoma wanavyotumia madawa ya kulevya

Aidha Bwn, Elianza Ngoda  amefafanua juu uhusiano uliopo kati ya marumizi ya dawa za kulevya na changamoto ya afya ya akili.

Pichani Bwn. Elianza Ngoda akifafanua uhusiano kati matumizi ya madawa ya kulevya na afya ya akili