Dodoma FM

Mradi wa bwawa kuipaisha Swaswa kiuchumi

1 October 2024, 7:53 pm

Na Mindi Joseph.

Ujenzi wa eneo la mapumziko katika Bwawa la Swaswa Jijini Dodoma unatarajiwa kuwanufaisha wananchi kiuchumi.

Bwn. Isaack Daniel ambaye ni mjumbe na pia msimamizi wa ulinzi na usalama katika mtaa wa Swaswa amezitaja fursa za kiuchumi zinazotokana na mradi wa ujenzi wa bwawa hilo ni pamoja na ajira  kwa wakazi wa Swaswa.

Pichani Mjumbe anayesimamia ulinzi na usalama katika mtaa wa Swaswa Bwn.  Isaack Daniel
Sauti ya Bwn.  Isaack Daniel

Mwenyekiti wa Mtaa wa Swaswa Charles Nyuma amesema kuwa hatua zilizofikiwa hadi sasa ni pamoja na  kukamilika kwa mchakato wa kuanza ujenzi kwa wananchi waliokuwa wanajishughulisha na kilimo cha mboga mboga  katika bwawa hilo kuridhia ujenzi kufanyika.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Swaswa Charles Nyuma
Sauti ya Bwn, Charles Nyuma
Pichani ni shughuli za ulimaji wa bustani za mbogamboga eneo la mradi