Dodoma FM

Miundombinu wezeshi inahitajika Viziwi kushiriki chaguzi zijazo

1 October 2024, 7:54 pm

Na Mariam Matundu

Kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa kundi la viziwi bado linatajwa kuachwa nyuma katika kushiriki mchakato huo kutokana na changamoto ya mawasiliano.

Hii ni kutokana na uhaba wa wakalimani wa lugha ya alama katika mchakato huo wa uchaguzi pamoja na imani potofu kwa jamii juu ya viziwi.

Mariam Matundu amefanya mazungumzo na katibu wa chama cha viziwi  mkoa wa Dodoma CHAVITA , Bwn. Ally Jumanne ambapo ameanza kumuuliza ushiriki wa viziwi katika mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ukoje?

Pichani Bi. Mariam Matundu akifanya mahojiano na katibu wa chama cha viziwi  mkoa wa Dodoma CHAVITA , Bwn. Ally Jumanne
Sauti ya Bi. Mariam Matundu na Bwn. Ally Jumanne