Dodoma FM

Chidachi walilia urasimishaji wa makazi

30 September 2024, 7:09 pm

Na Nazael Mkude .

Wakazi wa Chidachi Kusini Mkoani Dodoma wameomba kupata huduma ya  upimaji  wa viwanja pamoja na kurasimishiwa makazi yao ambayo wamekuwa  wakiyatumia kwa muda mrefu.

Wakieleza malalamiko yao kupitia  kituo cha habari cha Dodoma TV, wamesema  kuwa  kutokana na kutorasimishwa kwa maeneo yao wanashindwa kuyaendeleza   ili kupata makazi bora.  

Bi Maria Permena Mwanza mkazi wa Chidachi Kusini
Sauti za wanachi
Bwn, Shabani Kayanda mkazi wa Chidachi Kusini

Mwenyejiti wa Mtaa wa Chidachi Kusini Bwn. Mohamedi Ramadhani amesema kuwa kunachowashangaza ni kuwa wapo waliopata hati za umiliki wa maeneo hayo kupitia kampuni za upimaji ilihali wananchi wanaohudumiwa na vyombo vya serikali wakiwa hawajui ni lini watapata huduma hiyo.

Mwenyejiti wa Mtaa wa Chidachi Kusini Bwn. Mohamedi Ramadhani
Sauti ya Bwn. Mohamedi Ramadhani

Dodoma TV ilifanya jitihada kumtafuta Mkuu wa Divisheni ya Uendelezaji ya Makao Makuu  Bwn. Maduhu Ilanga kuzungumzia suala hili kwa isivyobahaiti hakupatikana.