Dodoma FM
Wanne mbaroni tuhuma za mauaji Dodoma
30 September 2024, 7:11 pm
Na Nazael Mkude.
Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za matukio ya mauaji yaliyofanyika kwa nyakati na muda tofauti ndani ya Jiji la Dodoma.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma George Katabaz amesema kuwa maeneo yalikotokea mauaji hayo ni pamoja na Mahomanyika Nzuguni, Mbuyuni Kizota, Mkonze na Segu Bwawani Nala.