Dodoma FM

RC Dodoma: Hakuna nyongeza ya siku uandikishaji daftari la wapiga kura

24 September 2024, 8:31 pm

Yussuph Hassan.

Wananchi mkoani Dodoma wamehimizwa kushiriki katika kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura kuanzia Septemba 25 hadi Oktoba 1.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema kuwa baada ya muda uliotolewa kuisha hakutakuwa na nyongeza ya siku za uboreshaji wa taarifa katika daftari la mpiga kura.

Sauti ya Mhe. Rosemary Senyamule

Aidha Senyamule ametaja vituo vitakavyotumika katika zoezi hilo kwa kila wilaya.

Aidha wananchi Jijini Dodoma wameeleza utayari wa kushiriki zoezi hilo pamoja na faida zake.

Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura litahusisha waliotimiza umri wa miaka 18 na kuendelea na watakaotimiza miaka 18 kabla ya tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, waliohama kutoka katika vituo walivyojiandikisha awali, waliopoteza sifa, wenye taarifa ziizokosewa na waliopoteza kadi au kuharibika.

Dodoma Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule katika picha ya pamoja na wadau na waandishi wa habari.