Serikali kudhibiti wizi wa vifaa vya ujenzi uwanja wa ndege Msalato
24 September 2024, 8:31 pm
Na Mindi Joseph
Udokozi na wizi wa vifaa vya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa Msalato Jijini Dodoma umesababisha hasara kwa mkandarasi.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe. Jabiri Shekimweri anasema serikali haitafumbia macho wizi wa vifaa vya ujenzi uliofanyika katika stoo ya kuhifadhia viafaa ya mkandarasi anayejenga uwanja wa ndegewa kimataifa Msalato jijini Dodoma.
Aidha Meneja wa Wakala wa Barabara TANROADS Mkoa wa Dodoma Mhandisi Zuhura Amani anasema pamoja na jitihada mbalimbali wanaweka mifumo thabiti ya wizi kutofanyika tena.
Ujenzi huo ulioanza Novemba mwaka 2022 unahusisha sehemu mbili upande wa majengo na miundombinu ambapo sehemu ya ujenzi wa majengo imefikia asilimia 43.6 na Miundombinu ni asilimia 75.8.