Utaratibu wa daftari la makazi kinga dhidi ya mauaji Dodoma
20 September 2024, 7:50 pm
Na Nazael Mkude
Wakazi jijini Dodoma wametoa maoni yao kuhusu utaratibu wa kujiandikisha katika daftari la makazi ili kuweza kupunguza vitendo vya uvunjifu wa sheria.
Kufuatia mwendelezo wa matukio ya kihalifu ya mara kwa mara yanayotokea katika jiji la Dodoma, wananchi wameiomba serikali kurudisha utaratibu wa kujiorodhesha katika daftari maalum la makazi.
Aidha wenyeviti wa mitaa pamoja na mabalozi wamesema kuwa ili kupunguza mauji na matukio yanayotokea kwa baadhi ya maeneo ya jiji la Dodoma utaratibu wa daftari la makazi utasaidia kuwatambua wakazi husika pamoja na wageni wanaohamia au kuishi kwa muda katika maeneo ya makazi.
Maoni ya kurejeshwa kwa utaratibu wa daftari la kudumu la mkazi yanatokana na kujitokeza kwa matukio ya mauaji na uhalifu ya mara kwa mara katika jiji la Dodoma.