Dodoma FM

Mauaji ya kutisha Mkonze

6 September 2024, 9:03 pm

Mauaji ya kutisha Mkonze

Watu wawili wa familia moja ambao ni mama na mtoto wameuawa usiku wa kuamkia leo na watu wasiofahamika kata ya Mkonze mtaa wùua Muungano Dodoma.

Na Nazaeli Mkude

Watu wawili wa familia moja ambao ni Mama na mtoto wameuawa usiku wa kuamkia leo na watu wasiofahamika baada ya kuvamiwa ndani ya nyumba walimokuwa wamelala katika mtaa wa Muungano B, Kata ya Mkonze, Jijini Dodoma.  

Watu waliouawa katika tukio hilo wamefahamika kwa majina ya Mwamvita Mwakibasi pamoja na Salma Ramadhan.

Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo akiwemo Juma Radhamn pamoja na Pendo Mwakabasi ambao ni ndugu wa marehemu , wanasimulia jinsi walivyopata taarifa ya kuuawa kwa ndugu yao na jinsi walivyokuta hali ilivyokuwa baada ya mauaji hayo kutokea.

Sauti ua dada wa Marehemu – Pendo Mwakabasi
Sauti ua dada wa Marehemu – Pendo Mwakabasi
Sauti ua kaka wa Marehemu – Juma Ramadhani

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mkonze David Bochela amesema mikakati waliyonayo katika kuimarisha ulinzi ili kudhibiti matukio ya uhalifu.

Sauti ya Diwani Kata ya Mkonze – David Bochela
Sauti ya Diwani Kata ya Mkonze – David Bochela
Baadhi ya majirani wakiwa wamekusanyika makundi makundi nyumbani kwa marehemu Mwamvita Mwakibasi