Historia ya kilimo cha Zabibu
29 November 2023, 3:21 pm
Dodoma ndio mkoa pekee unaolima Zabibu kwa wingi nchini Tanzania na hata kwa afrika mashariki ndio mkoa wenye utajiri mkubwa wa zao hili.
Na Yussuph Hassan.
Kilimo cha Zabibu mkoani Dodoma kina historia ndefu, ambapo kwenye miaka ya 1950 na mwaka 1974 chini ya uzaidizi wa bihwana misheni, serikali ya Tanzania wakati huo ikishirikiana na serikali ya china ilianzisha kituo cha kilimo cha Bihawana Farmers Training Center (BFTC) kwa ajili ya kufundisha Wakulima juu ya kilimo cha Zabibu na mazao mengine.
Dodoma ndio mkoa pekee unaolima Zabibu kwa wingi nchini Tanzania na hata kwa afrika mashariki ndio mkoa wenye utajiri mkubwa wa zao hili.
kuna maeneo mengi yanayolima zabibu mkoa wa dodoma
kuna aina tatu za Zabibu ambazo ni Zabibu za mvinyo,Zabibu za mezani na Zabibu za kukausha ambazo zote zinazalishwa Dodoma na katika aina hizo kuna aina zaidi ya 20 za zabibu zinazolimwa dodoma leo fahari ya dodoma imetembelea kituo cha utafiti wa kilimo tari makutupora kufahamu kwa kina juu ya zao hili.