Viongozi watakiwa kuacha kutumia nguvu za giza
9 October 2023, 8:36 pm
Wito huo umetolewa na Askofu wa Kanisa la Pentecoste Christian International Thomas Kiula wakati wa tukio la Uzinduzi wa kanisa jipya na kumsimika Uchungaji wa kanisa hilo linalopatikana mtaa Ndachi kata ya Mnadani Dodoma Mjini.
Na Seleman Kodima.
Viongozi wametakiwa kuacha kutumia Nguvu za Giza wakati wakisaka nafasi ya Uongozi kupitia Chaguzi mbalimbali hapa nchini .
Akizungumza baada ya tukio hilo Askofu Kiula amesema wakati Taifa tunaelekea uchaguzi wa mwaka 2024 ipo haja Viongozi wanaotumia Nguvu za giza kuanza kubadilika na kumtegemea Mungu ili kuwa na Utawala Bora wenye hofu na Mungu.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika Tukio hilo Diwani wa Kata ya Mnadani Paul Richard ambaye aliwakilishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Aman Bw Mussa Daudi amesema viongozi wa Dini wana nafasi kubwa ya kuombea Taifa na Viongozi.
Aidha amewataka Vijana kufanya kazi kwa bidii ili waweze kumtolea Mungu sadaka.
Nae Mchungaji wa kanisa hilo ambaye amesimikwa Henry Masunyilo amewashukuru waumini wa kanisa hilo pamoja na wananchi wa eneo hilo kwa upekee na ushirikiano walionesha katika tukio hilo adhimu.
Katika Uzinduzi huo ,Askofu wa Kanisa hilo amefanya harambee ya Viti ambapo Jumla ya Viti 47 viliweza kutolewa na baadhi ya Viongozi wa Kidini pamoja na serikali ambapo Diwani wa kata ya Mnadani ameahidi kutoa shilingi laki Tano .