Jamii yatakiwa kujenga mazoea ya kutumia maziwa
30 August 2023, 4:58 pm
Daktari Malaki amesema kuwa maziwa hayasaidii kusafisha mfumo wa hewa kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakiamini.
Na Aisha Alim.
Jamii imeshauriwa kujenga mazoea ya kunywa maziwa mara kwa mara ili kuimarisha afya zao kutokana na maziwa hayo kuwa na virutubisho muhimu kwa mwili wa binadamu.
Hayo yameseemwa na Daktari Malack Malack alipokuwa akizungumza na Dodoma tv na kuwataka wananchi kutumia maziwa kwani yanaimarisha kinga ya mwili na kuondoa hatari ya uzito mwilini.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na kituo hiki juu ya mwenendo wa utumiaji maziwa licha ya kutambua faida zake kiafya pia wameeleza kutokuwa na desturi ya kunywa mara kwa mara kutokana na sababu.
Hata hivyo daktari Malaki amesema kuwa maziwa hayasaidii kusafisha mfumo wa hewa kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakiamini juu ya dhana hiyo.