Dodoma wafurahishwa ongezeko la mtama sokoni
29 August 2023, 4:32 pm
Kutokana na Shirika la Afya , mtama umeweza kuwa chakula muhimu katika kupambana na changamoto ya udumavu pamoja na unyafunzi kwa watoto.
Na Astedi Bambora.
Upatikanaji wa zao la mtama kwa wingi katika soko kuu la majengo Jijini Dodoma kumewanufaisha wananchi wengi .
Wakizungumza na Taswira ya Habari, baadhi ya wananchi wamesema kuwa kutokana na zao hilo kupatikana kwa wingi kumerahisisha hali ya upatikanaji wa chakula na hapa wanabainisha matumizi mbalimbali ya zao hilo.
Taswira ya Habari imezungumza na Bw. Fadhiri Saidi ambaye ni mfanyabiashara wa zao hilo Soko kuu la Majengo amethibisha kuwa Mtama umekuwa unapatikana kwa wingi hasa Dodoma vijijini hali ambayo imesababisha Mtama kusafirishwa hadi nje ya nchi.
Nao baadhi ya wananchi wameshauri kuwa jamii ijitahidi kulima Mtama kwani unahimili ukamewa Mvua chache hata hivyo soko lake limekuwa linapanda zaidi.