

17 August 2023, 2:02 pm
Mfumo wa stakabadhi za Ghala umechangia ukusanyaji wa fedha kuwa rahisi kwa Halmashauri na Wakulima.
Na Mindi Joseph.
Jumla ya mazao 13 nchini yametajwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani ikiwa ni hatua kubwa kutoka mazao machache ndani ya miaka 3 iliyopita. Hii ni kufuatia uhamasishaji wa matumizi ya mfumo huu kwa wananchi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala nchini Asangye Bangu amebainisha hayo Jijini Dodoma na hapa anaeleza tija ya urasimimishaji wa mfumo huo.
Katika Mwaka wa fedha 2022/23 kilogram milioni 370 zimepita katika mfumo huo.