Baba, mama lishe watakiwa kuzingatia usafi
10 August 2023, 2:28 pm
Watoaji wa huduma ya vyakula katika maeneo mbalimbali ikiwamo migahawa na hotel wanashauriwa kuwa katika hali ya usafi ikiwemo uvaaji wa mavazi nadhifu ili kulinda afya ya walaji.
Na Mariam Msagati.
Usafi binafsi kwa wafanyabishara wanaojihusisha na biashara ya kuuza chakula maarufu kama Baba lishe na mama lishe umetajwa kama moja ya mambo ya msingi ya kuzingatia ili kufanya biashara hiyo katika hali ya mvuto na afya bora.
Dodoma tv imewatembelea baadhi ya mama lishe katika eneo la majengo jijini Dodoma na hapa wanaeleza umuhimu wa kutumia mavazi maalum kwa ajili ya kujisitiri katika biashara hiyo.
Baadhi ya wateja wanasema kuwa upo umuhimu wa wafanyabishara hao kutumia mavazi maalumu kwani yanaashiria kuwa wanazingatia swala la usafi binafsi, usafi wa mazingira yanayo wazunguka pamoja na kuvutia wateja.
Bi Rhoda Boi ni mwenyekiti wa kamati ya afya na mazingira katika soko kuu la majengo Jijini Dodoma anaeleza umuhimu wa wafanyabishara wa vyakula pamoja na wauzaji wa nyama kuvaa mavazi meupe na kofia ili kulinda afya za walaji.