Mlimwa walalamikia upungufu wa huduma ya maji
2 August 2023, 2:59 pm
Ngulelo amesema kuwa hali hiyo inawalazimu kutumia maji ambayo si safi na salama na kuiomba Serikali kuingili kati suala hilo.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa kijiji cha Mlimwa wilayani Chamwino wamelalamikia changamoto ya upungufu wa huduma ya maji hali inayowapa wakati mgumu Wazee,watu wenye Ulemavu na wanawake.
Wakizungumza na Taswira ya Habari baadhi ya wananchi wameiomba Wakala wa Usambazaji maji vijijini RUWASA kuwasaidia kuwapeleka mradi wa maji utakaosaidia kutatua adha hiyo.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Musa Ngulelo amesema kuwa kisima kilichopo hakikidhi mahitaji ya vitongoji vyote hali inayosababisha baadhi ya wananchi kutembea umbali mrefu.
Ngulelo ameongeza kuwa hali hiyo inawalazimu kutumia maji ambayo si safi na salama na kuiomba Serikali kuingili kati suala hilo
Simoni Macheho ni Diwani wa Kata ya Membe amesema tayari kijiji cha Mlimwa kipo kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 ili kuondokana na changamoto ya maji