Wadau na wananchi watakiwa kushiriki katika utekelezaji mpango wa Ardhi
14 July 2023, 7:33 pm
Mradi huu wa Uboreshaji usalama wa milki za ardhi unagharamiwa na Serikali kuu kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na katika Halmashauri ya Wilaya ya chamwino Mradi huo utatekelezwa katika vijiji 60 vilivyopo wilayani humo
Na Seleman Kodima.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe Gift Msuya amewataka wadau pamoja na wananchi kushiriki vyema katika utekelezaji wa mpango wa matumizi ya ardhi kupitia mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi
Mkuu huyo wa Wilaya ameyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa wadau wa kujadili mpango wa matumizi ya ardhi wilaya ya chamwino ambapo amesisitiza umuhimu wa utekelezaji wa mpango huo wa matumizi ya ardhi wilaya utasaidia kuleta matokeo chanya katika kuchochea maendeleo ya wilaya hiyo.
kwa upande wake Meneja wa Urasimishaji ardhi Vijijini kupitia mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi Bw Joseph John Osena amesema mpango huo kwa wilaya ya chamwino una lengo la kubaini aina kuu tatu za ardhi .
Sauti ya Meneja wa Urasimishaji ardhi Vijijini .