Zaidi ya shilingi millioni 300 kujenga miundombinu ya maji Kigwe
4 July 2023, 4:39 pm
Wazawa wametakiwa kupewa kipaumbele zaidi katika miradi mbalimbali inayo anzishwa wialayani humo.
Na Bernad Magawa
Zaidi ya Shilingi million 300 zinatarajiwa kujenga miundombinu ya maji katika kata ya kigwe ili kuwaondolea changamoto ya kukosa maji safi wananchi wa kata hiyo iliyowasumbua kwa miaka mingi huku visima 8 vikitarajiwa kuchimbwa vijiji mbalimbali ndani ya wilaya ya Bahi.
Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya vyeti kama ishara ya kuanza kutekelezwa kwa miradi ya maji, Mgeni wa heshima katika hafla hiyo Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bahi Stuwart Masima amewaagiza watumishi wa serikali kuhakikisha wanawasaidia wakandarasi ili kukamilisha mirad hiyo kwa wakati.
Nao viongozi mbalimbali walioshiriki hafla hiyo wakiwemo Mbunge wa Jimbo la Bahi Mhe Kenneth Nollo pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Mhe. Donald Mejiti (MNEC) wamezungumzia miradi hiyo huku Kaimu Mkurugenzi wa wilaya ya Bahi Denis Komba akielekeza wazawa kupewa kipaumbele katika kazi ndogondogo kwenye miradi hiyo.
Awali meneja wa Ruwasa wilaya ya Bahi Robert Mgombela alieleza namna miradi hiyo itakavyotekelezwa huku wakandarasi watakaojenga miradi hiyo wakiishukuru serikali kwa kuwaamini na kuahidi kutekeleza miradi hiyo kwa wakati nao wananchi wa kata ya kigwe wakifurahia kupelekewa maji.