Nollo atatua changamoto ya huduma za afya Mapinduzi Kigwe
4 July 2023, 3:49 pm
Uwepo wa huduma za afya kwenye kila kijiji wilayani Bahi mkoani Dodoma kutawahakikishia wananchi wa wilaya hiyo usalama wa afya zao pindi watakapopatwa na maradhi mbalimbali.
Na Bernad Magawa.
Mbunge wa jimbo la Bahi Mhe. Kenneth Nollo ametoa zaidi ya shilling million 16 katika ujenzi wa zahanati ya Mapinduzi kata ya Kigwe ili kuwaondolea changamoto wananchi wa kijiji hicho kufuata huduma za afya umbali mrefu.
Akizungumza wakakati wa kikao kwenye kata ya Kigwe Mheshimiwa Nollo amesema pamoja na mfuko wa jimbo halmashauri ya wilaya ya Bahi pia imepanga kupeleka fedha kwa mwaka huu wa fedha kuhakikisha zahanati hiyo inakamilika ili kuanza kutoa huduma.
Nollo amesema kwa muda wa miaka miwili ambao yeye amekuwa madarakani kama Mbunge wa Jimbo la Bahi, amebakisha vijiji viwili tu kati ya 16 ambavyo havikuwa na huduma za afya wakati anaingia madarakani huku akiahidi kukamilisha vjijiji vyote kabla ya 2025.