Serikali yaondoa tozo miamala ya kutuma fedha kwa njia ya simu
27 June 2023, 6:28 pm
Mkoa wa Dodoma umebahatika kupata minara 36 huku 6 ikijengwa na Vodacom.
Na Mindi Joseph.
Serikali imeondoa tozo kwenye miamala ya kutuma fedha katika mitandao mbalimbali ya simu ili kuondoa adha kwa watazania.
Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye katika uzinduzi wa ofisi mpya za Vodacom jijini Dodoma amesema Rais Samia ameridhia kuondoa tozo za kutuma miamala kwa njia ya simu hadi asilimia 0.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso amesema sekta ya mawasiliano inatengeneza uchumi wa nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amebainisha kuwa mkoa wa Dodoma umebahatika kupata minara 36 huku 6 ikijengwa na Vodacom
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Vodacom Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema Vodacom wamepeleka minara hadi vijijini ili kurahisi mawasiliano kwa wananchi na kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.