NEMC, TBS zakutana kujadili katazo vifungashio vya plastiki
26 June 2023, 1:37 pm
Vifungashio visivyo kidhi ubora vinatajwa kuleta athari katika mazingira.
Na Fred Cheti.
Baraza la uhifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) limekutana na shirika la viwango nchini (TBS) na kufanya kikao kazi kwa lengo la utekelezaji wa katazo la matumizi ya vifungashio visivyokidhi ubora.
Akizungumza mara baada ya kikao hicho mkurugenzi wa uzingatiaji na utekelezaji wa sheria za mazingira kutoka katika baraza hilo Bi. Redempta Samuel ameelezea lengo la kuwa na kikao hicho.
Kwa upande wake afisa viwango kutoka katika shirika hilo la viwango nchini (TBS) Bwana Henry Msuya anaelezea jinsi ambavyo wamepanga kushirikiana na (NEMC) katika kupunguza matumizi ya vifungashio ambavyo vinatajwa kuwa na athari katika mazingira.