TMDA yakabidhi dawa na vifaa tiba kwa mkuu wa Gereza la Msalato
16 May 2023, 6:00 pm
Vifaa tiba na Dawa zilizokabidhiwa leo na TMDA vimetokana na kaguzi zilizofanywa na Mamlaka hiyo na kuondosha katika soko la dawa ambayo vinafaa kwa matumizi lakini kwa mujibu wa sheria ya dawa na vifaa tiba ,dawa havikupaswa kuuzwa ama kutumika katika maeneo husika .
Na Seleman Kodima.
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba kanda ya kati TMDA leo imekabidhi Vifaa tiba na Dawa vyenye thamani ya shilingi Milioni 15 .599 kwa Mkuu wa Gereza la Msalato ili viweze kutumika katika zahanati ya gereza la Msalato.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika zahanati ya Gereza la Msalato na Meneja wa TMDA kanda ya Kati BI Sonia Henry Mkumbwa na Mkuu wa Magereza Msaidizi na Mganga wa Zahanati ya Gereza la Msalato ,Mrakibu wa magereza Dkt Abuusalami Mpamba ikiwa ni muendelezo wa TMDA Kanda ya Kati ikiendelea na utekeleza majukumu yake lengo likiwa ni kulinda afya ya jamii.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Meneja wa TMDA kanda ya kati Bi Sonia amesema kuwa hatua ya kutoa msaada huo ni baada ya kakugizi walizofanya awali na kuona hali ya miundombinu ya zahanati ,wahudumu ,mfumo wa utunzaji wa nyaraka.
Kwa upande wake Mkuu wa Magereza Msaidizi na Mganga wa Zahanati ya Gereza la Msalato ,Mrakibu wa magereza Dkt Abuusalami Mpamba akizungumza kwa Niaba ya Mkuu wa Gereza na Kamishina jenerali wa Magereza Tanzania amesema kuwa kupitia dawa hizo watahakikisha zinawafikia walengwa ili kuwatibu na kuwaponya.
Nao baadhi ya Wanajamii wanaopata huduma katika Zahanati hiyo akiwemo Anjela Kimario,Prisca Paulo na Ovidio Francis wamesema msaada huo utakuwa tumaini la upatikanaji zaidi wa dawa na vifaa tiba na itapunguza changamoto kwenye huduma za msingi za Mama na Mtoto.