Wasimamizi ujenzi wa kituo cha Afya Nkuhungu wapewa wiki tatu kukamilisha
27 April 2023, 6:13 pm
Kituo hicho pindi kitakapokamilika kinatarajia kuhudumia zaidi ya wananchi elfu 40 wa kata ya Nkuhungu.
Na Fred Cheti.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mh Jabir Shekimweri amewataka wasimamizi wa ujenzi wa mradi wa kituo cha afya Cha Nkuhungu ndani ya wiki tatu wawe wamehakikisha kituo hicho kinaanza kutoa huduma kwa wananchi.
Mh. Shekimweri amesema hayo leo wakati akiweka jiwe la Msingi Katika Kituo hicho ambacho awali kilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi kama zahanati kabla ya halmashauri ya jiji la Dodoma kuunga mkono juhudi hizo na kutoa fedha ili mradi huo ujengwe kama kituo cha afya.
Kituo hicho pindi kitakapokamilika kinatarajia kuhudumia zaidi ya wananchi elfu 40 wa kata ya Nkuhungu kama anavyosoma taarifa ya mradi huo Bi Mwasiti Abdala ambae ni Afisa mtendaji wa Kata ya Nkuhungu.
Kwa upande wake diwani wa Kata ya Nkuhungu Bwn. Mkhandi Daudi Nae alikua na haya kuelezea kuhusu uwepo mradi huo wa kituo cha afya katika kata yake.