Dodoma FM
Wananchi watakiwa kutambua kilimo cha umwagiliaji ni cha uhakika
24 April 2023, 4:04 pm
Dodoma ni miongoni mwa mikoa iliyo na hali ya ukame na Hupata wastani hali inayopelekea kulima mazao yanayostahili ukame kama vile uwele, mtama, mahindi, karanga, alizeti, ufuta na zabibu.
Na Mindi Joseph.
Wananchi Kata ya Babayu wamehimizwa kujikita katika kilimo cha umwagiliaji ambacho uzalishaji wake ni wa uhakika.
Taswira ya habari imezungmza na Mwenyekiti wa kijiji cha Kogongo Daudi Mohamed ambapo amesema serikali inafanya jitihada kubwa za kuboresha miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji hivyo ni wakati wa wakulima kujikita katika kilimo hicho kutokana na Mvua kusuasua.
Katika hatua nyingine amesema mashamba ya wakulima yataongezewa thamani kupitia kilimo cha umwagiliaji.