Wafanyabiashara wa mbogamboga walalamika bishara ngumu
19 April 2023, 5:42 pm
Hii inafuati msimu wa mvua za mazika ambazo zimekoma hivi karibuni Mkoani hapa hivyo watu wengi wenye maeneo wameotesha mbogamboga mbalimbali na kuzipa kisogo mbogamboga za sokoni.
Na Thadei Tesha.
Wafanyabiashara wa mbogamboga wamelalamikia kudorola kwa soko la mboga hizo kutokana na wanunuzi wengi kuotesha mboga nyumbani.
Licha ya kushamiri kwa mbogamboga sokoni bado hali ya upatikanaji wa wateja sio ya kuridhisha je nini sababu inayopelekea changamoto hiyo baadhi ya wauzaji wa bidhaa hiyo wanaeleza zaidi
Aidha kwa upande wao baadhi ya wananchi jijini Dodoma wanasema kuwa kufuatia msimu wa mvua kumepelekea watu wengi kupanda mbogamboga majumbani hivyo kupelekea mwitikio wa kununua mboga hizo kuwa mdogo.
Katika baadhi ya masoko jijini Dodoma upatikanaji wa bidhaa za mbogamboga ikiwemo tembele mchicha na chinese imeonekana kushamiri zaidi kwa hivi sasa.