Dodoma FM
Wananchi Membe watarajia kunufaika na kilimo cha umwagiliaji
28 March 2023, 4:46 pm
Na Mindi Joseph
Ujenzi wa Bwawa la kilimo cha umwangiliaji Membe Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma umefikia asilimia 35 huku ujenzi huo ukitarajiwa kukamilika mwezi Augosti 2023.
Taswira ya Habari imezungumza na Mhandisi Saleh Ramadhan ambaye ni msimamizi mkuu wa ujenzi wa bwawa hilo ambapo amesema bwawa hilo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji ujazo wa lita Bilioni 12.
Amesema Ujenzi huo ulianza mwaka 2022 na unatumia miezi 12 ili kukamilika.
Wananchi wanasema watanufaika kutokana na bwawa hilo.
Bwawa hili litakidhi mahitaji ya kilimo cha umwagiliaji ambapo itajengwa pia skimu yenye ekari elfu nane pamoja na matumizi ya nyumbani.