Uhaba wa wachangia Figo waendelea kuwa kikwazo
13 March 2023, 5:49 pm
Mpaka sasa Hospitali ya Benjamin Mkapa imefanikiwa kupandikiza Figo wagonjwa 33 kati ya hao wagonjwa 22 walipandikizwa Figo na wataalamu wazawa.
Na Mindi Joseph.
Ukosefu wa wachangiaji Figo umetajwa kuendelea kuwa kikwazo kwani Wananchi wengi hawapo tayari kujitolea kuchangia Ndugu zao.
Hayo yamebainishwa Leo Mkurungezi Mtendaji wa Hospital ya Benjamin Mkapa Dkt Alphonce Chandika katika maadhimisho ya miaka 5 ya upandikizaji Figo katika Hospital hiyo.
Amesema katika miaka mitano wamegundua kuwa wananchi hawapo tayari kuchangia Figo.
Kwa upande wake Neema Sweti Mkazi wa ihumwa Jijini Dodoma anaeleza ilivyojitolea kuchangia Figo huku Faraji Shaban aliyefanikiwa kupandikizwa Figo akaipongeza serikali
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, UDOM, Prof. Lughano Kusiluka naye amesema.