Wizara ya ardhi yaanza majarabio usalama wa milki za ardhi
24 February 2023, 3:05 pm
Mradi wa uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi una lengo la kwenda kuongeza idadi ya miamala itokanayo na nyaraka za umiliki.
Na Selemani Kodima
Wizara ya ardhi kupitia ofisi ya Ardhi mkoa wa Dodoma imeanza majaribio ya mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi katika mtaa wa Bihawana kata ya Mbabala jijini Dodoma .
Kazi mfano (Pilot) imeanza jana huku jiji la Dodoma likiwa ni sehemu ya Mpango wa ambapo kata ya kwanza kati ya zile imekuwa ni Mbabala ndani ya mtaa (Bihawana)
Hayo yamebainishwa na Meneja Urasimishaji wa ardhi mijini ambae pia ni Mpimaji mkuu wa ardhi kutoka wizara ya ardhi Bw Leons Peter Mwenda wakati akizungumza na wakazi wa mtaa wa Bihawana ambapo ameeleza lengo la Mradi huo na yapi ambayo wananchi wanatakiwa kushiriki katika utekelezaji wa mradi huo.
Kwa upande wake Afisa mipango miji kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bi Anna Nade amesema zoezi hilo litawezesha kutambua kila kipande cha ardhi hivyo mwananchi anatakiwa kuonesha ardhi yake na mipaka ya eneo lake.
Naye Afisa Mazingira katoka Halmashauri ya jiji la Dodoma Ally Mfinanga amesema katika hatua ya utambuzi na upimaji wa ardhi hawategemei kupima eneo ambalo ni chanzo cha maji,maeneo ya hifadhi ,milima huku pia akizungumzia maeneo ya pembezoni mwa barabara yataoteshwa miti .
Mradi wa uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi una lengo la kwenda kuongeza idadi ya miamala itokanayo na nyaraka za umiliki, kupunguza muda unaotumika kupata nyaraka za milki, kuongeza uelewa wa usalama wa milki kwa kuzingatia jinsia, kuongeza idadi ya watanzania wanaomiliki nyaraka za umiliki pamoja na kuongeza ufanisi utakaofanya wamiliki kuridhika na mchakato wa uandaaji nyaraka za umiliki