Urasimishaji ardhi ni changamoto kwa wananchi wasio kuwa na elimu juu ya zoezi hilo
10 August 2022, 2:33 pm
Na; Victor Chigwada.
Pamoja na faida za urasimishaji na upimaji wa ardhi nchini lakini zoezi hili limekuwa na changamoto kadhaa wa kadha kwa baadhi ya maeneo kutokana na uelewa mdogo wa wananchi
Taswira ya habari imezungumza na Jane samsoni ambaye amekiri licha ya zoezi la urasimishaji na upimaji viwanja kukamilika lakini kumekuwa na mkanganyiko kwa wananchi Hali inayosababisha kuibua migogoro
.
Bi Samsoni ameiomba Serikali kupitia Halmashauri kuingilia Kati zoezi Hilo kwani wananchi wengi wanalalamika kuonewa na kuchukuliwa viwanja vyao
.
Aidha mjumbe mwakilishi wa kitongoji Cha Ndwene Bw.Gidioni Nyagalu amekiri kukumbana na changamoto ya uelewa wananchi juu ya suala la upimaji viwanja hali inayochagia kukosekana kwa barabara za mitaa
.
Ameongeza kuwa pamoja na zoezi Hilo kupokelewa na wananchi lakini mizozo imekuwa mingi kutokana na baadhi ya wananchi viwanja vyao kuhamishwa .
.