Ukosefu wa ajira chanzo cha matumizi ya dawa za kulevya
16 March 2022, 1:43 pm
Na; Elizabeth Japhet.
Ukosefu wa ajira unatajwa kuwa moja ya sababu inayosababisha baadhi ya vijana kujihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya.
Bwana Swaleh ni miongoni mwa wahanaga wa dawa za kulevya na mfanyabiashara wa soko kuu la majengo jijin Dodoma amesema vijana kutokujishughulisha na kazi kunasababisha kujiunga na makundi mabaya na kujihusisha katika matumizi ya dawa za kulevya.
Aidha mfanyabiashara huyo amesema kuwa baadhi ya wazazi wanawatenga watoto wao hivyo husababisha vijana kujiunga na makundi yanayojihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya kutokana na upweke wanaoupata kwa wakati huo.
Kwa upande wake mshauri wa waathirika wa dawa za kulevya Bwana Christian Mlelwa kutoka jijini Dodoma amesema ni muhimu wazazi kufatilia hatua kwa hatua mienendo ya vijana wao ili kuwaepusha na matumizi ya dawa za kulevya.
Matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana inachangia kuzorotesha maendeleo ya kiuchumi ndani yaTaifa ambapo Serikali inaendelea kupambana kuzuia uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya nchini.