Rais Samia Suluhu apokea Ujumbe Maalumu kutoka kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame
4 June 2021, 9:39 am
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kumkaribisha Mjumbe Maalumu wa Rais wa Rwanda Paul Kagame, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda Dkt. Vincent Biruta mara baada ya kuwasili Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma jana tarehe 03 Juni, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Rwanda Paul Kagame, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda Dkt. Vincent Biruta mara baada ya kuwasili Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma jana tarehe 03 Juni, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisoma Ujumbe huo Maalumu wa Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasilishwa kwake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda Dkt. Vincent Biruta Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma jana tarehe 03 Juni, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Rwanda Paul Kagame, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda Dkt. Vincent Biruta wapili kutoka (kushoto) wakwanza (kulia) ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na wakwanza kushoto ni Balozi wa Rwanda hapa nchini Meja Jenerali Charles Karamba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiagana na mgeni wake Mjumbe Maalumu wa Rais wa Rwanda Paul Kagame, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda Dkt. Vincent Biruta mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.