Changamoto ya Madawati shule ya sekondary Wotta yatatuliwa
27 April 2021, 10:00 am
Na; Seleman Kodima
Wakazi wa kata ya Wotta wilayani Mpwapwa wameishukuru Dodoma fm redio kwa Juhudi ya kubwa walizofanikisha kuripoti tatizo la uhaba wa madawati ktika shule ya sekondari na hatimaye Changamoto hiyo kufanyiwa kazi .
Hayo yamejiri baada ya kituo hiki kuripoti changamoto ya uhaba wa madawati katika shule ya sekondari Wotta inavyoathiri ukaaji na umakini wa watoto wawapo darasani.
Wakizungumza na Taswira ya habari baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema zoezi la kutatua changamoto ya madawati shuleni hapo limekwisha anza ambapo mafundi wana endelea na zoezi la utengenezaji wa Viti na meza .
Nae Diwani wa kata hiyo Bw. Mugabe Athumani amesema zoezi la utengenezaji wa Viti na meza linaendelea huku wananchi wa Vijiji vyote ndani ya kata yake wakishiriki kikamilifu katika hatua zote za utengenezaji madawati hayo .
Aidha amewataka wananchi kuendelea kuchangia michango mbalimbali pale inapohitajika kuhusu masuala mbalimbali ya kimaendeleo ndani ya kata yao.
Hivi karibu Taswira ya habari iliripoti kuhusu uhaba wa madawati katika shule ya wotta hali ambayo imefanyiwa kazi na Uongozi wa kata hiyo kwa kushirikiana na wananchi.