Dodoma FM
Dodoma FM
25 March 2026, 17:06

Mbio hizo za marathoni zinatarajiwa kukusanya jumla ya shilingi milioni 100.
Na Mariam Kasawa.
Mbio za Marathoni zilizoandaliwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) linatarajiwa kufanyika katika Jiji la Dodoma 04/04/2026 huku mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa.
Akizungumza na wanahabari hii leo, Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC), Agnes Mtawa alisema kuwa lengo la marathoni hiyo ni kukusanya fedha kwaajili ya kuwajengea uwezo wauguzi na wakunga pamoja na wataalam wengine wa afya wanaotoa huduma katika vyumba vya upasuaji kwenye hospitali za halmashauri na vituo vya afya vinavyotoa huduma ya upasuaji hapa nchini.
Alisema kuwa mbio hizo zinatarajiwa kuhamasisha utoaji huduma kwa kuzingatia maadili ya kitaaluma ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma yenye kuzingatia heshima na utu
marathoni hii tuliyoandaa itawaleta pamoja wakimbiaji watakaokimbia katika umbali wa KM 5, 10 na 21na inatarajiwa kuwa mbio hizi kubwa zitajumuisha takribani wakimbiaji 2,000 ambao kila mmoja atashiriki kwa mchango wa shilingi 30,000″ alisema Mtawa.