Dodoma FM

Muungano wataka kukamilika jengo la mama na mtoto

25 March 2026, 16:43

Wameiomba Serikali kuingilia kati ili ujenzi wa jengo la mama na mtoto uweze.Picha na mtandao.

Amekiri kusimama kwa ujenzi wa jengo la mama na mtoto ambalo limefikia kwenye hatua ya kupaua lakini ujenzi umekwama kwa sasa.

Na Victor Chigwada.

Wananchi wa vitongoji vya Ilolo na Muungano wilayani Chamwino wameiomba Serikali kuingilia kati ili ujenzi wa jengo la mama na mtoto uweze kuharakishwa  ili kupunguza adha Kwa akina mama wajawazito

Wamesema kuwa kutokana na ujenzi wa jengo hilo kuchelewa kumepelea akina mama wajawazito kujifungulia kwenye wodi za wagonjwa wa kawaida jambo ambalo si salama kiafya.

Sauti wananchi.

Nae Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw.Matonya Mtukamsihi amekiri kusimama kwa ujenzi wa jengo la mama na mtoto ambalo limefikia kwenye hatua ya kupaua lakini ujenzi umekwama kwasasa.

Sauti Bw.Matonya Mtukamsihi

Mtukamsihi ameongeza kuwa licha ya uwepo wa mikataba ya wadau wa madini mchanga lakini fedha hizo pia zinategemewa kwenye ujenzi wa sekondari na kupelekea kukwama kwa  ujenzi wa jengo la mama na mtoto .

Sauti Bw.Matonya Mtukamsihi