Dodoma FM

Serikali kutoa ajira kwa Maafisa ustawi wa jamii kwenye maeneo yenye uhitaji

25 March 2026, 11:40

Picha ni Naibu WaziriOfisi ya Waziri Mkuu Kazi, ajira na Mahusiano Mhe. Rahma Kisuo alipokua akifungua Kongamano la siku tatu. Picha na Mkoa wa Dodoma.

Elimu na masuala ya Mifumo rasmi ya Serikali ambapo wameajiriwa katika ngazi zote za Serikali ikiwa ni pamoja na Vijiji, Kata, Wilaya, Mkoa, Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali.

Na Mariam Kasawa.
Serikali imesema itaendelea kutoa ajira kwa Maafisa Ustawi wa Jamii kwenye maeneo yenye upungufu mkubwa hususan Zahanati na Kata kwani Kada hiyo ni ya Muhimu kwa ustawi wa jamii.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Rahma Kisuo alipokua akifungua Kongamano la siku tatu na Mkutano wa Mkuu wa mwaka 2026 na Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Ustawi wa jamii lililoandaliwa na Chama cha Maafisa Ustawi wa Jamii Tanzania (TASWO) na kufanyika katika ukumbi wa Lavenda Jijini Dodoma.

Picha ni baadhi ya washiriki wa ufunguzi wa Kongamano la siku tatu na Mkutano Mkuu wa mwaka 2026 na Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Ustawi wa jamii.Picha na Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bw. Mussa Mkamati amesema Maafisa ustawi wa jamii wana jukumu la kumfikia mwananchi wa chini kwenye jamii na kumpatia huduma zinazostahili na Wizara yake ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria, Sera, Miongozo na mikakati.

Aidha, akisoma risala ya Chama mbele ya mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Ustawi wa Jamii Tanzania (TASWO) Dkt. Mariam Makuu, amesema Kongamano hilo litawakutanisha wanataaluma wote wa Kada hiyo ambapo watajadili kwa pamoja masuala ya Kitaalam kwa lengo kuu la kuboresha Elimu, Sera na huduma za ustawi wa nchi.

TASWO kilianzishwa mwaka 1982 kwa Sera ya usajili wa Vyama vya ndani lengo kuu likiwa ni kuunganisha nguvu za Wanachama wanaotoa huduma za ustawi wa jamii kwa kufanya ushawishi, utetezi na kusimamia misingi na maadili ya Kitaaluma katika utoaji wa huduma.