Dodoma FM

Wasio ripoti kidato cha kwanza wasakwa kurejea shuleni

24 March 2026, 17:33

Picha ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati akizungumza na Maafisa Elimu Msingi na Sekondari,Maafisa Utumishi,Watendaji wa Kata na Maafisa elimu Kata.Picha na Mkoa Dodoma.

Pamoja na wale wote ambao kwa mujibu wa maoteo walipaswa kuandikishwa darasa la awali na darasa la kwanza, lakini hawajaandikishwa, waweze kupelekwa shule.

Na Mariam Kasawa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewapa siku 07 Maafisa Elimu Kata na Watendaji Kata kuhakikisha wanawatafuta watoto wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2026 ambao bado hawajaripoti shule ,pamoja na wale wote ambao kwa mujibu wa maoteo walipaswa kuandikishwa darasa la awali na darasa la kwanza, lakini hawajaandikishwa, waweze kupelekwa shule kwani haki ya kupata elimu ni ya kila mtoto.

Mhe Senyamule ameyasema hayo leo Machi 23,2026 wakati akizungumza na Maafisa Elimu Msingi na Sekondari,Maafisa Utumishi,Watendaji wa Kata na Maafisa elimu Kata katika kikao kazi chake alichokiitisha kwa lengo la kuzungumza na Watendaji hao,sambamba na kuweka mikakati ya pamoja ya kuongeza ufaulu wa Mkoa.

Sauti ya mh. Rosemery Senyamule.