Dodoma FM

Wananchi Mpwapwa wapitisha mpango matumizi bora ya ardhi

24 March 2026, 16:59

Picha ni wananchi wa wilaya ya Mpwapwa wakiwa katika mkutano huo .Picha na Steven Noel.

Mpango huo umepitishwa katika vijiji vya Lukole, Mzase, Kingiti, Iyenge, Kidenge, Mgoma, Nzogole na  kitati ikiwa ni mwendelezo wa serikali  kuhakikisha vijiji vyote nchini vinapangwa, kupimwa na kumilikishwa.

Na Steven Noel.

Wananchi wa vijiji nane vya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wamepitisha mpango wa matumizi bora ya ardhi pamoja na sheria ndogo za kusimamia utekelezaji wake.

Mpango huo una lengo  kupunguza migogoro ya ardhi kati ya wakulima, wafugaji na kudhibiti uvamizi wa maeneo na kupunguza uharibifu wa mazingira

Kazi ya kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa vijiji hivyo imefanywa na wananchi   kwa kushirikiana wataalam wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi   na  wataalam kutoka Halmashauri ambapo baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo wamesema mpango utawasaidia kulinda maeneo yao ya ardhi .

Picha ni wananchi wa wilaya ya Mpwapwa wakiwa katika mkutano huo .Picha na Steven Noel.

Baadhi  ya Wananchi wa Kijiji cha mzase a wamesema mpango huo utasaidia kuchochea maendeleo Katika vijiji hivyo na kupunguza migogoro inayotokana na mwingiliano wa matumizi ya ardhi,

Nae Afisa ardhi  kutoka tume ya MATUMIZI ya ardhi amesema kuwa mpango hu ni mkombozi  wa mabadiliko ya tabia ya nchi na uhifadhi wa mazingira na  katika kupata haki ya umiliki wa ardhi

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo  bwana Baraka Habari   ameeleza umuhimu wa mpango huo kwa wananchi na serikali .

Sauti ya Noel kina.