Dodoma FM
Dodoma FM
06/03/2026, 17:16

Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria ni taasisi ya serikali inayosimamia rasilimali za maji katika bonde la Ziwa Victoria upande wa Tanzania,Taasisi hii inahakikisha matumizi ya maji yanafanyika kwa njia endelevu.
Na Bernard Komba.
Bodi ya maji bonde la ziwa Victoria imefanikiwa kutoa zaidi ya vibali 1000 katika maeneo tofauti lengo ikiwa kusimamia matumizi sahihi na endelevu kwa kuzingatia sheria na sera ya maji nchini yam waka 2000 toleo jipya la 2025.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo March 6,2025 mkurugenzi wa bodi hiyo DKT Renatus Shinhu amesema moja ya majukumu ya bodi hiyo ni kuhakikisha wanatoa vibali kwa watu kuendana na miongozo ya sera ya maji kulingana na matumizi ya binadamu Pamoja na mazingira.
Ameongeza kuwa sera na sheria ya maji inaelekeza bodi hiyo kutazama eneo la kiuchumi ikiwepo viwanda Pamoja na umwagiliaji wa mashamba.

Akizungumzia miradi mingine ambayo inatekelezwa na bodi yay a maji bonde la ziwa Victoria amesema ni Pamoja na kujenga mabwawa katika sehemu mbalimbali ambapo hadi hivi sasa wamefanikiwa kujenga mabwawa 7
Aidha amesema bodi imefanikiwa kuweka mipaka katika vyanzo vya maji 25 ili kutunza na kulinda upatikanaji wa maji katika ziwa Victoria.
Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria ni taasisi ya serikali inayosimamia rasilimali za maji katika bonde la Ziwa Victoria upande wa Tanzania,Taasisi hii inahakikisha matumizi ya maji yanafanyika kwa njia endelevu, salama na yenye manufaa kwa wananchi, mazingira na Uchumi Bonde hili linahusisha maeneo yanayozunguka Ziwa Victoria, ziwa kubwa zaidi barani Afrika,Katika upande wa Tanzania linajumuisha mikoa kama Mwanza, Kagera, Geita, Simiyu na sehemu za Shinyanga