Dodoma FM

Uhaba wa nguzo chanzo Mapinduzi A kukosa umeme

04/03/2026, 17:42

Idadi ya watumishi kwasasa ni ndogo ukilinganisha na idadi ya wahitaji wa huduma ya umeme.

Wamejitahidi kufuatilia mamlaka husika lakini utekelezaji ndio umekosekana na kupelekea nishati ya umeme kuendelea kuwa ni miongoni mwa changamoto kubwa Kwa wakazi wa Mapinduzi A.

Na Victor Chigwada.

Wakazi wa Mtaa wa Mapinduzi A wamepaza sauti juu ya uhaba wa nguzo za umeme Hali inayo pelekea wananchi wengi kushindwa kunufaika na huduma ya nishati ya umeme.

Miongoni mwa wakazi hao wameeleza namna ambavyo wananchi wamekuwa na shauku ya kutumia nishati hiyo lakini uhaba wa miundombinu ni changamoto.

Wamesema kuwa idadi ya watumishi kwasasa ni ndogo ukilinganisha na idadi ya wahitaji wa huduma ya umeme kwani wachache waliopo karibu na Barabara ndio wa nufaika wa nishati hiyo ya umeme.

Aidha wameiomba Serikali kuweka mpango wa kuongeza usambaaji wa miundombinu ya umeme Ili watu wengi waweze kunufaika.

Sauti za wananchi

Mwenyekiti wa mtaa huo Bw.Golden Mathayo amekiri uwepo wa kilio Cha wananchi juu ya kukosa nishati ya umeme

Bw.Golden Mathayo