Dodoma FM
Dodoma FM
04/03/2026, 16:30

Semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo viongozi wa makundi katika maeneo ya uongozi itifaki,elimu ya fedha ,urasimishaji pamoja na matumizi sahihi ya fursa mbalimbali kuelekea Tamasha la 17 la muziki wa kitamaduni wa asili ya chigogo.
Na Anwary Shaban.
Baraza la sanaa la Taifa BASATA limetoa wito kwa wasanii wote nchini kujirasimisha kupitia mfumo wa mtandaoni ili waweze kutambulika kisheria na kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali.
Wito huo umetolewa wilayani Chamwino mkoani Dodoma na Afisa sanaa wa BASATA,Angela Mhilu,wakati wa semina kwa viongozi wa makundi yatakayoshiriki Tamasha la 17 la muziki wa chigogo.
Mhilu amesema wasanii wanapaswa kutumia mfumo wa usajili unaopatikana kupitia kiungo cha Sanaa.go.tz ili kurasimisha kazi zao na kupata manufaa ya kisheria pamoja na fursa za maendeleo ya sanaa
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Naamala Samson amesema semina hiyo imewakutanisha viongozi takribani 60 kutoka makundi 50 yanayotarajiwa kushiriki tamasha hilo kwa lengo la kuwaimarisha katika maswala ya uongozi.
Naye Mratibu wa Tamasha la Muziki wa Chigogo Sospiter Makana amesema maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri huku zaidi ya makundi 50 yakitarajiwa kushiriki kwa mwaka huu ameongekuwa pamoja na burudani tamasha hilo litatoa ujumbe wa maadili na maendeleo kwa jamii.