Dodoma FM
Dodoma FM
17 February 2026, 5:12 pm

Mwananchi yeyote anao wajibu wa kutoa taarifa inayo muhusu kiongozi wa umma ambaye ameonesha mwenendo usio faa katika jamii na kiongozi huyo kuchukuliwa hatua za kinidhamu pindi atakapo gundulika kuwa ni kweli ametenda kosa la kimaadili.
Na Jerome John.
Wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano katika sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma pindi waonapo viongozi wanao kiuka misingi ya maadili.
Kwa mujibu wa ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianzishwa sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma yenye jukumu la kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi yeyote wa umma ambaye ameorodheshwa katika sheria ya maadili.
Aidha bwana Anno Mgani afisa kutoka ofisi ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma amesisitiza wananchi kutoa ushirikiano na kutokuwa waoga kwa kutoa taarifa za viongozi wanao kiuka misingi ya uongozi wa umma kuanzia ngazi za serikali za mitaa mpaka Taifa ili wachukuliwe hatua zinazo stahili.