Dodoma FM
Dodoma FM
16 February 2026, 4:14 pm

Dodoma media group mwaka 2026 iliamua kurejesha tabasamu kwa watoto hao wa kituo cha Quadiria kwa kupeleka mahitaji mbalimbali huku wakifurahi na watoto hao pamoja na wadau kwa kupata chai ya pamoja.
Na Mariam Kasawa.
Dodoma media group kwa kushirikiana na wadau februari 14 ilileta matumaini na faraja mioyoni mwa watoto wa Kituo cha Watoto Yatima wa kituo cha Quadiria kilichopo Ndachi Jijini Dodoma.
Kila februari 14 huwa ni maadhimisho ya siku ya wapendanao ambapo kila mtu huadhimisha siku hii kwa namna ya kipekee wapo ambao huadhimisha kwa kuwapa zawadi wenza wao kutoka na kutembelea sehemu mbalimbali na baadhi huadhimisha siku hii kwa kutoa sadaka kuwajali wenye uhitaji na kufurahi nao.
Akiongea baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali meneja wa Dodoma media Group Ibrahim Jamal aliwasihi wadau na wananchi kuendeleza upendo na kuwajali wahitaji kila wakati katika jamii.