Dodoma FM
Dodoma FM
12 February 2026, 2:37 pm

Magawa ameongeza kuwa njia sahihi ya kudhibiti wimbi Hilo la wizi ni pamoja na kuunda vikundi vya doria kwaajili ya kulinda Mali zao.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa kata ya Ihumwa walalamika mifugo inayopitishwa nyakati za usiku kwenda machinjioni wakidai kuwa huchanganywa kati ya mifugo halali na mifugo iliyo ibiwa kwa wananchi wa maeneo hayo.
Haya yanajiri siku chache baada ya wakazi wa eneo hilo kulalamikia wizi wa mifugo ambao umekuwa ukitokea katika eneo hilo mara kwa mara.
Kufuatia malalamiko hayo taswira ya habari imemtafuta Afisa mifugo wa Kata ya Ihumwa ili kutaka kujua ni utaratibu upi unaotumika Kwaajili ya ukaguzi wa mifugo inayo pelekwa machinjioni kwaajili ya kuchinjwa kila siku.
Bi.Genoveva Mihayo amesema kuwa kisheria hakuna utaratibu wa kusafirisha Mifugo usiku hususani wale walio kusudiwa kuchinjwa badala yake upo muda maalumu wa kuwasili na kuanza zoezi la uchinjaji .
Mihayo ameongeza kuwa kutembeza ng’ombe au mifugo mingine nyakati za usiku wa manane ni kosa kisheria hivyo mtu yoyote Anaye fanya hivyo anaweza kuziliwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Naye Diwani wa Kata ya Ihumwa Bw.Edwadi Magawa amewataka wananchi wa eneo hilo kujitolea kulinda mali zao ikiwemo kufanya doria za usiku pasipo kutanguliza maslahi binafsi .