Dodoma FM
Dodoma FM
10 February 2026, 10:57 am

Wananchi wa mtaa wa Bwawani wanaendelea kutoa wito kwa serikali za mitaa na mamlaka husika kuhakikisha miundombinu ya barabara inaboreshwa ili kuwawezesha kuendelea na shughuli zao kwa urahisi, hususan katika kipindi hiki cha mvua.
Na Anwary Shaban.
Wakazi wa mtaa wa bwawani kata ya Ipagala wameiomba serikali kuwasaidia kukarabati barabara za mitaa ambazo zimeharibiwa na mvua na kuwa kero kwao.
Wakiongea na Taswira ya Habari wanannchi hao wamesema kuwa barabara nyingi hazipitiki hususani msimu huu wa mvua hali inayosababisha usumbufu mkubwa katika shughuli zao za kila siku ikiwemo shida ya usafiri kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa mtaa wa Bwawani, John Komba, amethibitisha kuwepo kwa changamoto hiyo akisema kuwa ubovu wa barabara katika kata ya Kisasa umekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya wananchi.
Aidha, Komba amesisitiza umuhimu wa mshikamano kati ya viongozi wa ngazi ya kata na mitaa ili kuleta maendeleo kwa wananchi, akiwataka madiwani na wenyeviti wa mitaa kuepuka migawanyiko isiyo kuwa na tija.