Dodoma FM
Dodoma FM
30 January 2026, 1:46 pm

Picha ni Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri wakati akizungumza katika kikao cha Baraza la Biashara la Wilaya ya Dodoma. Picha na Dodoma City Tv.
Katika kikao hicho, Shekimweri amelipongeza baraza hilo kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya katika kuhamasisha uwekezaji na shughuli za kiuchumi.
Na Lilian Leopold.
Wananchi jijini Dodoma wametakiwa kuchamkia fursa mbalimbali za uwekezaji wa kibiashara zinazotokana na uboreshwaji wa mazingira ya uwekezaji unaondelea kufanyika jijini humo, hatua inayotarajia kuchochea ongezeko la wafanyabiashara na wawekezaji ili kukuza uchumi wa wilaya hiyo.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri wakati akizungumza katika kikao cha Baraza la Biashara la Wilaya ya Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri jijini Dodoma.
Kwa upande wao, Mwenyekiti wa Baraza la Biashara Ringo Iringo na Mjumbe wa sekta binafsi Idd Senge wamesema serikali inaendelea kutoa fursa kwa wawekezaji ili kuimarisha uchumi wa nchi.
Wamesisitiza umuhimu wa baraza hilo kuendelea kuwahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji kukutana mara kwa mara ili kujadili changamoto na fursa zilizopo, hatua itakayosaidia kuhakikisha huduma zote muhimu zinazohitajika zinapatikana kwa wakati na kuifanya Dodoma kuwa na mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji.